About
Tuliyokuandalia leo ni pamoja uchambuzi wa nusu fainali, mechi ya mshindi wa tatu na taarifa kuu kuhusu Kombe la Dunia kuhusu washindi kutuzwa pete pamoja na medali na kombe huku Ballon d'Or yatangaza mchezaji anayecheza nje ya Ulaya ana uwezo wa kushinda tuzo hiyo. Timu ya taifa ya kina dada ya Kenya na Tanzania zasafiri kwa ajili ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Morocco, fainali ya Congo Cup na washindi wa kombe la Afrika la vilabu mchezo wa handboli.