AFCON 2025: Morocco dhidi ya Comoros kufungua mashindano leo usiku
21 December 2025

AFCON 2025: Morocco dhidi ya Comoros kufungua mashindano leo usiku

Jukwaa la Michezo

About

Leo tunaangazia pakubwa kuanza kwa mashindano ya AFCON 2025; tunachambua mechi ya ufunguzi kati ya Morocco na Comoros, mjadala kuhusu mageuzi katika michuano hii, namna timu zilivyotua nchini Morocco kwa kuvalia mavazi ya kitamaduni, Morocco wapo kwenye shinikizo ya kunyakua ubingwa kwa kuwa mwenyeji lakini pia ubashiri wa mechi ya ufunguzi na atakayebeba taji la mwaka huu.