zeno
Home
Explore
Religious
Music
News
Podcasts
Bible
By Genre
By Location
By Language
Download App
Log in
Sign up
Toggle Sidebar
zeno
United Nations
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Daily News
Swahili
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Website
Episodes
100
03 December 2025
Guterres: Kunapokuwa na ujumuishwaji wa kweli kila mtu ananufaika katika jamii
Umoja wa Mataifa leo Desemba 3 unaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu kwa ujumbe mzito kutoka kwa Katibu Mkuu António Guterres ujumbe unaotaka jamii ziwe si tu zinazoweza kufikiwa na watuwenye ulemavu, bali pia zenye ujumuishi wa kweli. Flora Nducha na taarifa zaidi
2 min
03 December 2025
03 FEBRUARY 2025
Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu kuhusu siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu, simulizi ya Mwalimu mwenye ulemavu wa kuona na huduma za afya ya uzazi kwa wasichana vigori nchini Kenya.Umoja wa Mataifa leo Desemba 3 unaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu kwa ujumbe mzito kutoka kwa Katibu Mkuu António Guterres ujumbe unaotaka jamii ziwe si tu zinazoweza kufikiwa...
11 min
03 December 2025
Kuchukua hatua ya mpango wa uzazi kama msichana haimanishi unajihusisha na vitendo vya ngono kiholelaholela - Lucy
Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi UNFPA kupitia ufadhili kutoka kwa asasi ya Adolescent Sexual and #ReproductiveHealth Development Impact Bond, limewezesha wasichana nchini Kenya kupata huduma za uzazi wa mpango bila malipo, taarifa muhimu, na kufanya maamuzi sahihi na hivyo kulinda afya zao na kuboresha mustakabali wao. Sheilah Jepngetich anafafanua zaidi
3 min
02 December 2025
Jifunze Kiswahili: Maana ya methali "KOTI LA BABU HALIKOSI CHAWA"
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "KOTI LA BABU HALIKOSI CHAWA".
1 min
02 December 2025
02 DESEMBA 2025
Hii leo jaridani tukiendelea kukupa taarifa mbalimbali kuhusu siku 16 za kuhamasisha umma kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, leo tunaelekea Mjini Hoima Magharibi mwa Uganda kusikia hisia za wanawake kuhusu ukatili dhidi ya wanawake mtandaoni.Watu takribani 100,000 wamekimbia makazi yao kaskazini mwa Msumbiji ndani ya wiki mbili, huku Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR...
12 min
01 December 2025
UN: Dunia ipo katika kipindi cha maamuzi kuhusu mustakbali wa ukimwi
Kama tulivyokujuza le oni Siku ya UKIMWI Duniani na mwaka huu inaadhimishwa kwa onyo kali kuhusu janga hilo pamoja na wito wa kuchukua hatua. Ikibeba kaulimbiu “Kukabili misukosuko, kubadili mwelekeo wa hatua za UKIMWI,” Umoja wa Mataifa unasema dunia ipo katika kipindi cha uamuzi muhimu katika vita dhidi ya VVU. Flora Nducha na taarifa zaidi
2 min
01 December 2025
“VVU si mwisho wa maisha” – Safari ya Pooja Mishra kutoka mshtuko hadi uongozi
Pooja aliolewa akiwa na umri wa miaka 15, baadaye akiwa mdogo bado akagundua kuwa ana Virusi Vya Ukimwi, VVU, na leo ni Mratibu wa Kitaifa wa Vijana chini ya Muungano wa Kitaifa wa Watu wanaoishi na VVU nchini India (NCPI+), akifanya kazi moja kwa moja na zaidi ya vijana 1,800 kote India. Katika mahojiano yaliyofanywa na Anshu Sharma wa Idhaa ya Kihindi ya Umoja wa Mataifa, Pooja anasimulia...
3 min
01 December 2025
01 DESEMBA 2025
Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Siku ya UKIMWI Duniani, simulizi wa mwathirika wa ugonjwa huu amabye aliolewa na umri wa miaka 15, na juhudi za UNICEF Wajir nchini Kenya za kuhakikisha ujumuishwaji wa watoto wenye ulemavu darasani.Leo ni Siku ya UKIMWI Duniani na mwaka huu inaadhimishwa kwa onyo kali kuhusu janga hilo pamoja na wito wa kuchukua hatua. Ikibeba...
11 min
01 December 2025
UNICEF na KISE wawapiga jeki watoto wenye ulemavu katika Kaunti ya Wajir nchini Kenya
Katika Kaunti ya Wajir Kaskazini Mashariki mwa Kenya, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Maalum ya Kenya KISE wameanzisha mpango maalum wa kuwasaidia watoto wenye ulemavu kupata tathmini za kitabibu na kielimu. Mpango huu umeleta matumaini mapya kwa familia nyingi ambazo hapo awali zilikuwa na ugumu wa kupata huduma hizi kama anavyofafanua...
3 min
28 November 2025
Katibu Mkuu wa UN ameitaka Guinea-Bissau kurejesha utawala wa kikatiba mara moja
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amelaani vikali mapinduzi yanayoendelea nchini Guinea-Bissau akitaka “urejeshwaji wa haraka na usio na masharti wa utawala wa kikatiba” baada ya wanajeshi kutwaa madaraka kufuatia uchaguzi mkuu wa uliofanyika tarehe 23 Novemba. Selina Jerobon na maelezo zaidi.
2 min