
18 February 2026
Ushirikiano wa kikanda hatarini: Nakisi ya bajeti yaibua maswali mapya
Gurudumu la Uchumi
About
Juma hili tunajadili kuhusu mustakabali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, hasa wakati huu kukiwa na taarifa kuwa inakabiliwa na mgogoro wa kifedha.
Taarifa zinaonesha kuwa Jumuiya hiyo inakabiliwa na upungufu wa bajeti unaofikia karibu dola za marekani milioni 89, pengo ambalo huenda likatatiza shughuli za Jumuiya hiyo, jambo ambalo limemfanya rais wa Kenya William Ruto ambaye ni mwenyekiti wa jumuiya kwa sasa, kuitisha mkutano wa dharura wa wakuu wan chi mwezi ujao.