
03 December 2025
Ripoti ya Oxfam-Kenya: Uchumi unakua, lakini Wakenya wengi ni masikini, kwa nini?
Gurudumu la Uchumi
About
Msikilizaji juma lililopita shirika la kimataifa la kupambana na umasikini, OXFAM nchini Kenya, ilichapisha ripoti inayoonesha kuongezeka kwa pengo la usawa. Kwa mujibu wa shirika hilo, pengo la walionacho na wasio nacho linaendelea kuongezeka ambapo matajiri 125 wa Kenya kwa sasa wana utajiri wa zaidi ya watu milioni 42 raia wa Kenya.
Tunajiuliza, kwa nini ukuaji wa uchumi hauwahusu watu wengi?