About
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, nchi nyingi za Afrika zinakabiliwa na mzigo mkubwa wa madeni na gharama za juu za kukopa katika masoko ya kimataifa. Fedha nyingi ambazo zingetumika katika afya, elimu, miundombinu na ajira zinaishia katika kuhudumia madeni, hali inayoweka shinikizo zaidi kwa uchumi wa nchi hizi. Je, hitaji la Afrika la kuwa na mfumo mpya wa kifedha duniani wenye uwakilishi na usawa zaidi litawezekana?